Sheria inayoruhusu wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja, imepitishwa nchini Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria hio licha ya malalamiko kutoka kwa vikundi vya wanawake nchini humo.
Taarifa kutoka katika ofisi ya Rais
ilisema kuwa mswada huo ambao unaojumuisha vipengee kadhaa kuhusu ndoa ,
imekuwa sheria sasa.
Mswada huo ulioleta mageuzi katika sheria ya
sasa , ilipitishwa na bunge mwezi jana kuidhinisha rasmi utamaduni wa
ndoa ya zaidi ya mwanamke mmoja.
Taarifa ya Rais ilisema kuwa "ndoa ni muungano
wa watu wawili mwanamke na mwanamume , ikiwa mume atataka kuoa mke mmoja
au wawili, mwenyewe anapaswa kuamua. ''
Mswaa wa awali, ulimpa mwanamke haki ya kwenda
mahakamani kupinga mume wake kuoa mke wa pili, lakini wabunge wanaume
waliungana katika kuunga mkono mswada huo.
Wakati mswada huo ulipopitishwa mwezi jana , wabunge wanawake waliondoka bungeni kwa Hasira baada ya mjadala mkali.
Viongozi wa baadhi ya makanisa pia wamepinga vikali mswada huo
Shirikisho la kitaifa la mawakili wanawake pia limesema kuwa litapinga sheria hiyo mahakamani.
Katika sehemu nyingi barani Afrika, kuoa zaidi
ya mwanamke mmoja ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi sawa na
hali ilivyo nchini Kenya na hata pia miongoni mwa waumini wa dini ya
kiisilamu.
Wengi wanasema kuwa sheria hiyo inapiga tu muhuri wa utamaduni uliopo.
No comments:
Post a Comment