
Afisa Linda Okello akiwa kazini
Afisaa mmoja wa polisi mwanamke 
nchini Kenya amepewa onyo kali kwa kuvalia sketi iliyokuwa imembana 
kiasi cha kuonyesha umbo lake.
Wakuu wake walichukua hatua ya kumuonya polisi 
huyo baada ya picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na 
kupigiwa gumzo kubwa.
Alipigwa
 picha akiwa amevalia sketi yake fupi na yenye kumbana akiwa anashika 
doria katika eneo ambako mashindano ya magari yalikuwa yanafanyika eneo 
la Kati mwa Kenya.
Afisaa huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa 
kufika mbele ya mkuu wake James Mugeria na kuonywa vikali dhidi ya 
kuvalia hivyo kwa mara nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni 
utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya heshima kwa polisi
Maafisa mjini Kiambu walisema kuwa kupewa onyo 
kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya kuvalia sketi yake iliyokuwa 
imembana sana ni jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa kuendelea na 
majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti 
moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu. Lakini 
punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na
 baadhi wakiikejeli. 
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira 
kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa
 polisi kuvalia sketi ya kumbana. 
No comments:
Post a Comment