UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo 
wa mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa 
kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea 
ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki 
katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu 
yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua 
ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila 
iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom 
kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa
 mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za 
kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu 
nchini tumezishuhudia .Changamoto hizo ni ikiwemo upangaji wa ratiba 
usiyokuwa na uwiano mzuri,baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa
 mchezo,wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji 
wa tiketi,uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya 
kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka 
propaganda chafu na ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa 
ligi ndogo kama ya Tanzania. Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa 
baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1.    Klabu
 imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa 
timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na 
kununua basi kwa ajili ya matumizi mbalimbali  ya Halmashauri ikiwemo 
kutumiwa na timu zake
( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa 
basi hilo hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika 
gazeti la majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji  wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na 
wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja 
ya maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi la wachezaji  
taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa 
mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu.
2.    Propaganda
 kuwa Mwalimu Juma Mwambusi kanunuliwa nyumba Maeneo ya chamazi ili 
apange kikosi dhaifu siku ya mchezo tarehe 13/4/2014.
Mwalimu(Kocha) Juma Mwambusi ni muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la 
Mbeya,kwa maana hiyo ni mtumishi wa Umma. Mwalimu Mwambusi amekuwa na 
timu yetu kwa muda mrefu sasa na ataendelea kuwepo.Kumekuwepo na maneno 
yasiyofaa dhidi ya mwalimu wetu toka mzunguko wa pili wa ligi 
kuanza,maneno haya yamekuwa na nia ya kuaribu muenendo wa timu ili ianze
 kufanya vibaya lakini zaidi ya hapa yana nia ya kumdhalilisha mwalimu 
wetu na taaluma ya ukocha nchini.
Mwalimu amefedheheshwa  sana na taarifa hizo.
3.    Propaganda kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wamepewa hongo wacheze chini ya kiwango 13/4/2014.
Wachezaji ndiyo wachezaji wenye nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu 
ndani na nje ya uwanja muda wote,ni waadirifu na wanajua wanataka 
nini.Mpira ndiyo ajira yao kama watumishi wa umma ndani ya Halmashauri 
ya jiji la Mbeya.Hawajawahi na wala hawatawahi kuchukua rushwa kwa lengo
 la kupanga matokeo.
Klabu yetu haisadiki katika upangaji wa matokeo ya mchezo wa mpira wa 
miguu kwani tunajua fika kuwa hakutaisadia kama klabu lakini pia kama 
taifa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo wa mpira wa miguu una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka
 sare. Klabu inaamini kuwa timu iliyojiandaa vizuri kama yetu inastahili
 kupata matokeo mazuri uwanjani.Falsafa mojawapo ya timu yetu ni 
kushinda mechi kwa kucheza mpira unaovutia na kuwaburudisha watazamaji.
Tuhuma mbalimbali za upangaji matokeo katika ligi yetu zimeanza kuota 
mizizi hasa ligi inapoingia mzunguko wa pili ,katika suala hili kama 
ambavyo linataka kuhusishwa nasi yawezekana propaganda hizi kwa upande 
wa timu inayotuhumiwa kuandaa michakato hiyo wana uzoefu nalo na yumkini
 ndiyo chachu ya mafanikio yao mpaka kufikia hatua hiyo waliofikia sasa.
Kama timu hiyo inauwezo wa 
kirasilimali wa kufanya uovu huo wote iweje ishindwe kuwa na timu imara 
na ya ushindaji mpaka itegemee kutafuta wachezaji wa timu pinzani kupata
 matokeo mazuri?
Timu yetu ndiyo timu pekee changa miongoni mwa timu tano zinazoongoza 
msimamo wa ligi yetu kwa sasa,si hivyo tu bali ndiyo timu pekee 
inayoundwa na wachezaji wengi wapya katika ulimwegu wa soka na 
inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia wachezaji,benchi la ufundi 
pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa tunaweza kufanya kazi
 nzuri bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao wasiokuwa na tija.
Mpira ni ajira hatuna budi kuuratibu vema ili kutoa nafasi inayostahili 
kwa vijana wetu ili kupunguza tatizola ajira nchini lakini pia kutumia 
vipaji vyao kulipa taifa muonekano stahili.
Mamlaka zinazohusika hazina budi kuanza kufuatilia na kuchukua hatua 
kali kwa baadhi ya timu zinzohusishwa na upangaji wa matokeo ili kulinda
 heshima ya mchezo huo bila kuogopa uwezo wa rasilimali wa timu hizo.
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
9.04.2014

No comments:
Post a Comment