
Sabuni pia zinasemekana kuwa na kemikali zinazoathiri mbegu za wanaume
Kemikali zinazopatikana katika 
baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa kila siku kama vile dawa ya kusugua 
meno, sabuni na mafuta ya kujikinga kutokana na miale hatari ya jua 
zinaweza kuharibu mbegu za uzazi za wanaume.
Kwa mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa
 hizo zina uwezo wa kuanthiri uwezo wa mbegu za uzazi za wanaume 
kuzalisha mwanamke.
Wanasayansi hao wanasema kwamba 
bidhaa hizo zina kemikali ambazo zinachangia matatizo ya uzazi kwa 
wanaume katika nchi za magharibi.
Kemikali zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana kuharibu nguvu za mbegu za kiume kuweza kuzalisha.
Takriban mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa 
nchini Uingereza anakumbwa na tatizo la kuzalisha na tatizo la utasa 
ndio kiini kikubwa cha hali hiyo.
Uchunguzi huu ulifanywa na watafiti kutoka 
Uingereza na Uholanzi na walifanyia uchunguzi kemikali 100 kila siku 
huku wakigundua kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo ziliathiri uwezo wa 
Manii kufikia katika mayai ya mwanamke.

Dawa ya meno inaweza kuathiri mbegu za uzazi
Utafiti huu uliandikwa katika jarida la afya la 
EMBO na watafiti wanasema nyingi ya kemikali hizo hatari zinapatikana 
katika mafuta yanayotumiwa kujizuia na miale hatari ya jua. 
Kemikali nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana katika sabuni na dawa ya kusugua meno.
Uchunguzi wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri uwezo wa Manii ikitafuta mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha.
Kadhalika kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa hisia kwa homoni za mwanamke.
Mabadiliko haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa vigumu kuweza kuzalisha. Watafiti hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni hatari zaidi kwa mbegu hizo.
Kemikali hizi hujulikana kama kemikali 
zinazoathiri jinsia kwa sababu ni sehemu ya kemikali zinzzoathiri homoni
 za mwili wa mwanamume.
Mwaka jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani ya matiti na pumu.
No comments:
Post a Comment