Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez 
na klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya 
kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu ya Italia Giorgio 
Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.
Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.

No comments:
Post a Comment