KAMATI
 ya Uchaguzi ya Simba SC inapenda kuwaalika wanachama wote wa Simba 
katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliopangwa kufanyika Keshokutwa
 Jumapili, Juni 29 mwaka huu, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa 
Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Shughuli za uhakiki wa wanachama zitaanza saa moja kamili asubuhi na 
Mkutano umepangwa kuanza saa tatu kamili asubuhi na wanachama na 
wagombea wote wanaombwa kuwa wamekaa katika viti vyao kufikia muda huo.
Katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea 27 wanatarajiwa kushiriki na 
Kamati ya Uchaguzi imeazimia kwamba suala la muda litazingatiwa sana 
safari hii kutokana na ukweli wa kuwepo kwa wagombea wengi.
 
Ni matumaini ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kwamba wanachama watazingatia muda wa kufika ili kurahisisha shughuli za kamati.
 Kamati inatangaza pia kwamba katika uchaguzi huo, ulinzi utakuwa wa 
kiwango cha juu; ingawa ina matumaini kwamba wanachama wote watakuwa 
watulivu ili kulinda jina, heshima na hadhi ya Simba SC.
 
Benki ya Posta
 Wanachama wanatangaziwa kwamba kwenye uchaguzi kutakuwa pia na huduma 
ya kutoa kadi kwa washabiki wa Simba wanaotaka kuingia katika mfumo mpya
 wa Benki ya Posta. Simba na Benki ya Posta zimeingia katika 
makubaliano ya kutengeneza kadi hizo ambazo kwa utaratibu utakaotangazwa
 katika siku zijazo, ndiyo zitatumika kwa wanachama wote.
Uwanja Bunju
 Uongozi wa Simba unawakaribisha wapenzi na wanachama wake kesho Jumamosi katika Uwanja wa Klabu uliopo katika eneo la Bunju jijini Dar 
es Salaam kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa 
mazoezi wa klabu. Ujenzi huo ulioanza miezi miwili iliyopita, 
unakaribia kukamilika na utakuwa uwanja wa kwanza rasmi wa mazoezi wa 
klabu katika historia yake.Vyombo vya habari navyo vinaalikwa katika tukio hilo litakaloanza saa tano kamili asubuhi.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Katibu Mkuu
Simba SC

No comments:
Post a Comment