Huzuni:  Serge Aurier, Cheick Tiote na Didier Zokora wote walijumuika na kiungo huyo wakati wa huzuni kabla ya mchezo kuanza
Die
 alijaribu kuimba wimbo wa taifa lake, lakini kutokana na hisia kali 
alizokuwa nazo alishindwa kuzua machozi yaliyokuwa yanambubujika.
Beki Serge Aurier  na mchezaji wa zamani wa Tottenham, Didier Zokora haraka walienda kumfariji mwenzao kabla ya mechi kuanza.
 Nyota
 wa Newcastle, Cheick Tiote pia alienda kumpa mkono wa pole Die, ambaye 
kwa bahati mbaya mechi yenyewe ameshuhudia nchi yake ikifungwa mabao 
2-1.
James
 Rodriguez na Juan Fernando Quintero waliifungia Colombia wakati 
mchezaji wa zamani wa Asernal, Gervinho alifunga bao la kufutia machozi 
kwa Tembo.

Die mwenye machungu ya kufiwa na baba yake alicheza mechi dhidi ya   Colombia.




No comments:
Post a Comment