Marekani imeiwekea Uganda vikwazo kwa kupitisha 
sheria zinazopinga mapenzi ya jinsi moja katika taifa hilo la Mashariki 
ya Afrika. Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya 
usalama katika ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa 
barua kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Uganda 
mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.
                     
Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani. Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya. Aidha msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa 
usaidizi wa marekani pia utapunguzwa mbali na kufutiliwa mbali kwa 
mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya uganda na yale ya Marekani.
Sheria hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu 
wa jinsia moja na wale watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo cha 
maisha jela. Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda. Juma
 lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten Gillibrand alilalmikia
 vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya kigeni wa Uganda Sam Kutesa 
kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea 
Uganda. 

Marekani imeiwekea Uganda vikwanzo kuhusina na sheria ya wapenzi wa jinsia moja.
Watu 9000 walikuwa wametia sahihi pendekezo la 
kuitaka Umoja wa Mataifa kumng'oa kitini bw Kutesa aliyechaguliwa licha 
ya kampeini hiyo. Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wameenda 
mahakamani wakitaka sheria hiyo iondolewe lakini inatarajiwa kupingwa 
kwani rais Yoweri Museveni aliupitisha maksudi kudhihirishia wafuasi 
wake kuwa yu huru kutokana na shinikizo kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .
                     
Punde baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya 
benki kuu ya dunia iliahirisha utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo
 zilikuwa zinapaswa kutumika kuimarisha sekta ya Afya nchini Uganda .Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.

No comments:
Post a Comment