Baadhi ya viungo vilivyokutwa kwenye dampo hilo
POLISI mkoani Dar es Salaam wamekamata viungo mbalimbali vya
binadamu vilivyohifadhiwa katika mifuko ya plastiki katika dampo la takataka
lilipo maeneo ya Bunju B wilayani Kinondoni.Taarifa zinasema miili hiyo imeonekana ikiwa imetelekezwa
katika eneo hilo pamoja na kufungwa kwenye mifuko hiyo, ikiwa imekaushwa huku
baadhi ya viungo vikionekana kua vya watu wazima.
Akihojiwa na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Cammillius Wambura amethibitisha kukamatwa
kwa viungo hivyo. Kamanda Wambura amesema viungo hivyo vimepelekwa Muhimbili kwa
uchunguzi zaidi huku jeshi hilo likiendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini
ukweli wa tukio hilo.
Mguu wa binadamu ukiwa umechunwa ngozi
Tukio hilo lililoibua hisia kali kwa wananchi limesababisha
polisi kufyatua mabomu ya machozi kudhibiti wananchi waliofurika na kutaka
kuvamia kituo cha polisi kumkamata dereva wa gari lililokutwa na viungo hivyo.
Akizungumzia kuhusu dereva wa gari ambalo lilikuwa
linasadikiwa kubeba viungo hivyo, amesema kwamba watu wanachanganya habari,
dereva huyo alikuwa amebeba uchafu kutoka Interchick ambao ulikuwa unatoa harufu kali sana na
alikuwa anaenda kumwaga kwenye dampo hilo hilo. Kwa hiyo wananchi wakadhani
ndiye aliyetupa viungo hivyo na alikuwa anaenda kutupa kwa mara nyingine, hapo
ndipo baadhi ya wananchi wakambana dereva na kwenda kituo cha Polisi kilichopo
Bunju. Lakini baada ya polisi kukugaua uchafu uliobebwa kwenye gari hilo
waligundua kuwa sio viungo vya binadamu bali ni uchafu kutoka Interchick.
Gari linalosadikika kutupa viungo hivyo
Kamanda Cammillius Wambura amewaomba wananchi kuacha kueneza
habari ambazo hawana uhakika nazo katika
mitandao ya kijamii na kwingineko na badala yake wawaachie jeshi la polisi lifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment