Saturday, August 9, 2014

PROFESSOR JAY KUIRUDISHA TENA HARD BLASTERS CREW

 
Msanii mkongwe rapper Joseph Haule aka Professor J mzee wa mitulinga, amesema kundi lake la Hard Blasters Crew lipo mbioni kurejea tena.
Professor ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake ‘Tatu Chafu’, amedai kuwa members wengine wa kundi hilo, Fanani na Big Willy walikuwa wamebanwa na shughuli zingine lakini kwa sasa wapo tayari kurejea tena kwenye muziki.
“Wameshakuja, wananitembelea mara nyingi pale Mwanalizombe studios, tuna mipango kamilifu ya kufanya project nzito ya Hard Blasters,” amesema Professor.
“Fanani yupo, Big Willy wote wapo kwenye mood nzuri na muda si mrefu watawasikiliza Hard Blasters so tupo njiani na watu wapo around kwahiyo time imefika, studio tunayo na kila kitu, watu wategemee vitu vikubwa kutoka kwa Hard Blasters.
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...