Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO 
limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika 
mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani 
yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.
Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo 
likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo 
imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani 
mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.
Kuidhinisha utumizi wa dawa ilio katika majaribio ni swala gumu. Dawa hiyo ambayo haijajaribiwa imetumiwa na raia
 wawili wa kutoa msaada kutoka marekani ambao afya yao imeimarika,lakini
 kasisi huyo wa Uhispania ambaye pia aliitumia dawa hiyo ameaga dunia.
                     
Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi. Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza 
kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio iitwalo Zmapp baada ya
 kuiomba serikali ya Marekani. Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo.

Shirika hilo lilisema kuwa mahali ambapo 
matibabu ya majaribio yanapofanyiwa panahitaji kuwa na ridhaa na matekeo
 ya jaribio hilo kukusanywa na kushiriki na wengine.
                     
Katika ripoti iliyotolewa leo, shirika hilo 
linasema “Katika hali kama hizi za kuenea kwa ugonjwa huu, na iwapo 
masharti Fulani yataafikiwa, jopo hili limefikia makubaliano kuwa ni 
jambo la kimaadili kuingilia kati kwa mijarabu ambayo haijadhibitishwa 
huku ufanisi wake ukiwa haujulikani na adhari mbaya, kama matibabu au 
kinga.”
WHO ilitangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kama janga la afya la dharura ulimwenguni.
Huku hayo yakijiri, serikari ya Liberia imesema 
kuwa madawa yatakayofanyiwa majaribio yatafikishwa nchini humo baadae 
juma hili – ingawa watengenezaji wa dawa madawa hayo Mapp Bio 
pharmaceutical walikuwa wameonya kuwa madawa hayo ni haba.
Zmapp imetumiwa kuwatibu wafanyikazi wawili wa US aid ambao walionyesha dalili ya kupata nafuu.

Padri mmoja wa kanisa la Roman Catholic, 
aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini Liberia, na ambaye aliaga dunia 
baada ya kurejea nyumbani kwao nchuni Uhispania pia amedhaniwa kuwa 
alikuwa amepewa dawa hizo.
Hata hivyo, dawa hizo zimejaribiwa kwa nyani tu na bado haijatathminiwa kuwa ni salama kwa binadamu.
Shirika la afya dunini WHO linasema kuwa idadi 
ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa 
Africa sasa imepita watu 1000.
Hii leo wataalam hao wa WHO wamekubaliana kwamba
 utumizi wa dawa hizo utakubalika iwapo kutakuwa na uwazi huku rukhsa 
ikitolewa na wote wanaoshiriki katika tiba hiyo mbali na kuficha siri ya
 mgonjwa aliyetibiwa.
Na huku hayo yakijiri Liberia ambalo ndio taifa 
lililoathiriwa sana na ugonjwa huo lilianza kutumia dawa hizo kutoka 
marekani kabla ya uamuzi wa utumizi wake kutolewa na WHO.

No comments:
Post a Comment