Kama unadhani nyota Mario Balotelli anategemea soka tu
kuendesha maisha yake basi utakuwa unakosea. Blog yako ya Taswirabongo
inakupasha kwamba Mario Balotelli ni mbunifu pia na hivi karibuni amezindua
viatu vya soka vya watoto chini ya kampuni ya Puma. Viatu hivyo vimeandikwa
msemo ambao maarufu wa WHY ALWAYS ME?kwa nyuma pembeni ambao aliuandika kwenye
tshirt yake na kuunesha kwa mashabiki baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester
United wakati akiwa Manchester City. Pia kuna sahihi yake na huku vikipambwa
zaidi kwa kuwekwa style yake ya nywele maarufu kama kidiku kwa nyuma.
Ukiachana
na viatu pia kuna mipira ambayo imewekwa satyle yake ya ntwele ya kiduku. Viatu
vinauzwa Dola 50 na mipira ni dola 18 na kwa mujibu wa mauzo habari ni kwamba
mauzo yanaenda haraka sana kuliko ilivyotegemewa.
No comments:
Post a Comment