Thursday, August 27, 2015

Watu 9 wa familia moja wafariki dunia Buguruni Malapa kwa ajali ya moto



Habari zilizotufikia muda si mrefu kutoka East Africa radio kuna familia moja imeteketea kwa moto hapo Buguruni Malapa. Watu 9 wanasemekana wamefariki kasoro baba mwenye nyumba tu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo anasema kuna mtoto wa kiume alifanya ushujaa akafungua dirisha akarusha funguo za Geti nje ili watu wawafungulie lakini Geti ilikuwa tayari imeshika moto na haikuwezekana kabisa kusaidia chochote,

Taswirabongo inawapa Pole sana wafiwa wote na Mungu awape subra katika kipindi hiki kigumu.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...