MAMLAKA
ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za
kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February
mwaka huu ziko salama na sio za bandia ,huku asilimia 18 zikionekana
zikiwa za bandia hivyo kuwataka wananchi kutambua kuwa simu feki
zilizoko sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma.
Pia
imebainika kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua na umeme ni
kutokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa
kuhimili mionzi pindi zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha mlipuko
wa moto na hivyo kuleta madhara .
Hayo
yalisemwa na meneja uhusiano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania
Innocent Mungi alipokuwa akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi
ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyowashirikisha wadau na
wafanyabiashara wa jijini hapa.
Alisema
kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu
hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji
wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina
matatizo ya aina yeyote.
Alidai
kuwa kufuatia uzimaji wa simu bandia litakalofanyika juni 16 mamlaka
hiyo imeweza kutoa elimu kwa wauzaji,watumiaji ili kuhakikisha kuwa
wanabini simu zao kama ni salama ili kuweza kuepuka zoezi la kuzimiwa
simu zao bila yawao kujiandaa.
“Wakati
tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa asilimia 30
zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February simu
bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu feki
zilizoko sokoni ni chache mno “aliongeza .
Aidha
Innocent alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na
kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa
simu na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara
nyingi kwa njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.
Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba aliwataka wananchi kufanya
zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze
kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa
watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia .
Simba
aliseama kuwa ni vema wananchi wakatumia mfumo waliowekewa wa kubaini
simu zao kama ziko salama kwani ifikapo juni simu zote bandia zitazimwa
na kuwataka wafanyabiashara nao wawe makini pindi wanaponunua mizigo yao
ya bashara ili kuepuka hasara watakazozipata wao na pia hasara
watakazopata wanunuzi wa simu hizo
No comments:
Post a Comment