NAIBU waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo amewataka watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kuwa na utaratibu wa kutembelea maeneo yao ya kazi ili kujua changamoto zilizopo na kuzitatua.
Akizungumza na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B mkoani Dodoma
wakati wa ziara aliyoifanya Mheshimiwa Jafo amesema kuwa watumishi
hawawezi kufanya kazi kwa ubora iwapo hawatakuwa wakitembelea na kukagua
maeneo yao ya kazi.
Katika ziara yake amewataka walimu wa shule ya msingi Nzuguni B na
Shule ya sekondari Nzuguni A kuweka utaratibu wa kujiwekea malengo na
kujipima kuona walichokifanya ili kupata matokeo tarajiwa.
No comments:
Post a Comment