Saturday, April 23, 2016

Mafikizolo feat Diamond Platnumz & Dj Maphorisa - Colors Africa (Officia...

(OFFICIAL VIDEO)Lady jay Dee - NDI NDI NDI

GITAA KUACHIA AUDIO NA VIDEO MPYA KWA PAMOJA, MKONO WA ABY DADY


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Gitaa Supertalent ambaye alishawahi kusumbua na kibao chake matata sana kinachoitwa Homa ya Mapenzi hivi karibuni anatarajia kuachia ngoma mpya ambayo imesimamiwa na mikono salama ya mtayarishaji mkali wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo Aby Dady. Track hiyo mpya ipo katika hatua za mwisho ya kukamilika kwa video yake ambayo itakuwa na viwango vya kimataifa. 

Kwa mujibu wa Gitaa ambaye ni mkali wa masauti jina la track hiyo bado halijawekwa wazi ila ipo katika hatua ya mwisho kukamilika kwa hiyo wapenzi wa mziki mzuri wakae tayari kwa mkao wa kula kwa ajili ya kupokea mziki mzuri kutoka kwa kijana mwenye kipaji cha hali ya juu Gitaa Supertalent.



MBAO FC YA MWANZA YAPANDA LIGI KUU BARA(VPL) BAADA YA GEITA GOLD MINES KUSHUSHWA


Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) limeitangaza rasmi timu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza kupanda ligi kuu ya Tanzania Bara(VPL). Maamuzi haya yamefikiwa baada ya kamati ya nidhamu kuzishusha timu nne kutoka kundi C ambazo zilikutwa na hatia ya kupanga matokeo. Mbao FC imeongoza kundi hilo kwa pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu nne zilizokumbwa na mkasa huo ambazo ni Geita Gold Mine, Jkt Kanembwa, JKT Oljoro na Polisi Tabora.

Wakati huo huo kamati ya rufaa ya TFF inatarajia kukutana jumamosi ya tarehe 30 ya mwezi huu wa nne kujadili rufaa zilizokatwa na baadhi ya watuhumiwa. Waliokata rufaa ni Salehe Mang'ola, Yusuph Kitambo, Amosi Mwita, Fateh Remtullah, timu ya JKT Oljoro na Polisi Tabora.

Friday, April 22, 2016

BREAKING NEWS: UKAWA KUSUSIA BUNGE LA BAJETI




Umoja vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi maarufu kama UKAWA wametangaza kutochangia mjadala wa bajeti zote zinazoendelea ndani ya Bunge hadi pale serikali itakaporekebisha vipengele vinavyobana uhuru wa bunge kama vile urushwaji wa matangazo moja kwa moja na vyombo vingine bila vizuizi.

BARAKA DA PRINCE KUMSHIRIKISHA NAJMA KATIKA NGOMA YAKE MPYA


Staa wa muziki wa kizazi kipya Baraka Da Prince amesema ngoma yake mpya iitwacho ‘Twende’ ameimba kwa kumshirikisha mchumba wake Najma Dattan.
Staa huyo alisema kwamba kibao hicho tayari kimesharekodiwa na anatarajia kukisambaza kwenye vituo mbalimbalo vya redio nchini ili mashabiki wa muziki wa bongo flava waanze kuusikiliza.
”Sisi wote ni wasanii ndiyo maana tumeamua kushirikiana katika wimbo huu ambao una ujumbe maalum kwa Najma unaelezea safari ya kwenda kumtambulisha kwa wazazi wangu na tayari niemeshafanya hivyo,”alisema Baraka.
Msanii huyo aliongeza kwa kuwataka wale wanaozungumza taarifa za ‘Uzushi’ kuhusiana na maisha na mchumba wake waache kwa sababu kila anachokifanya na vitu anavyotumia ni mali yak na si via kuazima.
Baraka alisema kuwa wanaomsema vibaya ni wapinzani wake na hiyo haiwezi kumkatisha tamaa kwenye safari yao ya mafanikio waliyoianza

WATENDAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA WATAKIWA KUTEMBELEA MAENEO YAO YA KAZI




 NAIBU waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo amewataka watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa kuwa na utaratibu wa kutembelea maeneo yao ya kazi ili kujua changamoto zilizopo na kuzitatua.

Akizungumza na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B mkoani Dodoma wakati wa ziara aliyoifanya Mheshimiwa Jafo amesema kuwa watumishi hawawezi kufanya kazi kwa ubora iwapo hawatakuwa wakitembelea na kukagua maeneo yao ya kazi.
Katika ziara yake amewataka walimu wa shule ya msingi Nzuguni B na Shule ya sekondari Nzuguni A kuweka utaratibu wa kujiwekea malengo na kujipima kuona walichokifanya ili kupata matokeo tarajiwa.

ASILIMIA 79 ZA SIMU ZA MKONONI ZIPO SALAMA NA ASILIMIA 18 TU NDIO BANDIA



MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February mwaka huu ziko salama na sio za bandia ,huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia hivyo kuwataka wananchi kutambua kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma.

Pia imebainika kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua na umeme ni kutokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili  mionzi pindi zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha mlipuko wa moto na hivyo kuleta madhara .

Hayo yalisemwa na meneja uhusiano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Innocent Mungi alipokuwa akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya  namba za utambulisho wa simu za kiganjani iliyowashirikisha wadau na wafanyabiashara wa jijini hapa.

Alisema kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu  hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo ya aina yeyote.

Alidai kuwa kufuatia uzimaji wa simu bandia litakalofanyika juni 16 mamlaka hiyo imeweza kutoa elimu kwa wauzaji,watumiaji ili kuhakikisha kuwa wanabini simu zao kama ni salama ili kuweza kuepuka zoezi la kuzimiwa simu zao bila yawao kujiandaa.

“Wakati tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa asilimia 30 zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February simu bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache mno “aliongeza .

Aidha Innocent alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa simu  na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.

Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba aliwataka wananchi kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia .

Simba aliseama kuwa ni vema wananchi wakatumia mfumo waliowekewa wa kubaini  simu zao kama ziko salama kwani ifikapo juni simu zote bandia zitazimwa na kuwataka wafanyabiashara nao wawe makini pindi wanaponunua mizigo yao ya bashara ili kuepuka hasara watakazozipata wao na pia hasara watakazopata wanunuzi wa simu hizo 
 

Tuesday, October 20, 2015

Ronaldo, Messi, Neymar na Suarez watajwa katika orodha ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya Ballon d'Or 2015

 Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa dunia 2014 mapema mwaka huu

Full list of Ballon d'Or noiminees:
Sergio Aguero (Argentina/Manchester City)
Gareth Bale (Wales/Real Madrid)
Karim Benzema (France/Real Madrid)
Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid)
Kevin De Bruyne (Belgium/VfL Wolfsburg/Manchester City)
Eden Hazard (Belgium/Chelsea)
Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain)
Andres Iniesta (Spain/FC Barcelona)
Toni Kroos (Germany/Real Madrid)
Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich)
Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona)
Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona)
Thomas Muller (Germany/FC Bayern Munich)
Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich)
Neymar (Brazil/FC Barcelona)
Paul Pogba (France/Juventus)
Ivan Rakitic (Croatia/FC Barcelona)
Arjen Robben (Netherlands/FC Bayern Munich)
James Rodriguez (Colombia/Real Madrid)
Alexis Sanchez (Chile/Arsenal)
Luis Suarez (Uruguay/FC Barcelona)
Yaya Toure (Cote d'Ivoire/Manchester City)
Arturo Vidal (Chile/Juventus/FC Bayern Munich)

World Coach of the Year nominees:
Massimiliano Allegri (Italy/Juventus)
Carlo Ancelotti (Italy/Real Madrid)
Laurent Blanc (France/Paris Saint-Germain)
Unai Emery (Spain/Sevilla FC)
Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich)
Luis Enrique Martinez (Spain/FC Barcelona)
Jose Mourinho (Portugal/Chelsea)
Jorge Sampaoli (Argentina/Chilean national team)
Diego Simeone (Argentina/Atletico Madrid)
Arsene Wenger (France/Arsenal)

Washindi watatangazwa  tarehe 11 January 2016 mjini Zurich

Monday, August 31, 2015

Shilole akaidi adhabu ya Basata

Msanii Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amekaidi adhabu aliyopewa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) iliyomtaka kutoshiriki masuala ya sanaa ndani na nje ya nchi kwa mwaka mzima.
Msanii Shilole akifanya show katika jukwaa Mbeya ambapo alikuwa akimsindikiza Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dr. John Magufuli
Shilole amekaidi adhabu hiyo baada ya kuonekana akifanya show katika kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimnadi Mgombea nafasi ya urais wa chama hicho Dk. John Magufuli wakati wapo jijini Mbeya siku kadha zilizopita.
Kipindi cha Planet Bongo kilitaka kufahamu endapo adhabu ya msanii huyo imefutwa, na kuwatafuta Baraza la Sanaa Tanzania ndipo hapo Mama Sharua ambaye yupo katika Idara ya kukuza Sanaa na Masoko alipokanusha kufutwa kwa adhabu ya msanii huyo na kusema adhabu yake ipo palepale na kama amefanya shoo amekaidi adhabu hiyo.
"Shilole anatambua wazi kuwa anaadhabu hiyo hivyo kama amefanya shoo sisi kama Basata itabidi tukae chini na kufuatilia juu ya suala hilo na tukigundua kuwa kuna ukweli sheria itachukua mkondo wake," alisema Mama Sharua.
Basata imesema kitendo alichofanya msanii huyo ni wazi kuwa ameshindwa kuheshimu adhabu iliyotolewa na hivyo lazima sheria ichukue mkondo wake kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.
Planet Bongo ilimtafuta msanii Shilole kutaka kufahamu kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo ili hali anatambua kuwa anaadhabu ambayo inamkabili ndipo hapo msanii huyo aliposema kuwa tuyaache hayo mambo kwani ni mambo ya kiserikali zaidi.

CREDIT: www.eatv.tv
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...